<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>58</hymn_number>
<title>Mwamba Wenye Imara TZR58</title>
<lyrics>[V1]
 Mwamba wenye imara
 Kwako nitajificha!
 Maji hayo na damu
 Yaliyotoka humu,
 Hunisafi na dhambi,
 Hunifanya mshindi.

[V2]
 Kwa kazi zote pia ,
 Sitimizi sharia.
 Nijapofanya bidii,
 Nikilia nakudhii,
 Hayaishi makosa;
 Ndiwe wa kuokoa.

[V3]
 Sina cha mkononi,
 Naja Msalabani;
 Nili tupu, nivike;
 Ni mnyonge, nishike;
 Nili mchafu naja,
 Nioshe nisijafa.

[V4]
 Nikungojapo chini,
 Nakwenda kaburini;
 Nipaapo Mbinguni,
 Na kukwona enzini:
 Roho yangu na iwe
 Rahani mwako wewe.</lyrics>
</song>